Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Sababu Kumi (10) Zinazopelekea Wakamilishaji Kushindwa -1

Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea,

Sina uhakika kama itakufaa lakini ziko sababu nyingi zinazopelekea watu wengi wa mauzo kushindwa kukamilisha mauzo.

Eneo la kukamilisha mauzo ndiyo eneo ambalo watu wengi huwa wanaliogopa. Usiogope kumwambia mteja kinachofuata baada ya hapa ni wewe kulipia bidhaa au huduma unayotoa.

Hapa ni sababu tano ambazo mtu akiweza kuzivuka, ataweza kuwa na mafanikio makubwa kwenye ukamilishaji wa mauzo.

Moja, kutokujaribu kukamilisha.
Ni rahisi watu kuwaeleza watu kile wanachouza lakini cha kushangaza kinapofika kipindi cha kukamilisha mauzo watu wanaogopa.
Wateja hawatanunua mpaka wewe mwenyewe uwaambie wanunue.

Hatua ya kuchukua, kwenye mchakato mzima wa mauzo, hakikisha unawaambia wateja wanunue na uwasisitize hilo.
Kamilisha mauzo, mtenganishe mteja na fedha zake.

Mbili, kuona shinikizo ni baya.
Watu wamekuwa wana ustaarabu wa kijinga. Wanaogopa kuwaambia watu wanunue kwa sababu wataonekana ni watu wenye shinikizo. Na watu wanaona kumshinikiza mtu ni kitu kibaya.

Hatua ya kuchukua, ni wajibu wako kuhakikisha mteja anapata bidhaa au huduma unayotoa.
Hakuna ubaya wowote kama unamsaidia mtu kupata kitu kizuri. 
Hivyo wasisitize wateja wanunue kile unachouza kwa sababu ni kitu kizuri.

Tatu, kuepuka kuzikabili hisia.

Kwenye mauzo, kila mmoja ana kuwa na hofu yake.
Hofu ya kukataliwa kwa upande wa muuzaji na hofu ya kupoteza kwa upande wa mnunuaji.
Hisia hizi zinakuwa kikwazo kwa upande wa ukamilishaji wa mauzo.

Hatua ya kuchukua, kuwa na utulivu, usiruhusu hisia zikutawale katika mauzo.
Kuwa na utulivu mkubwa ili ukusaidie kufanya maamuzi sahihi.

Nne, kukosa imani kwenye bidhaa au huduma

Kama muuzaji unapaswa kuaminika. Unapaswa kuamini kile unachouza kiasi cha watu kutokuwa na shaka juu yako.

Wewe ndiyo uwe kinara namba moja wa kile unachouza. Usipokuwa na imani na kile unachouza, watu watashindwa kununua.

Ona ni wajibu wako kuhakikisha mteja anapata kitu kizuri kwa sababu kinakwenda kufanya maisha yake kuwa bora.

Tano, kutokuweka juhudi sahihi

Kila kitu kwenye maisha kinahitaji kazi.
Kitu chochote kwenye maisha huwa kinakuwa kigumu kama utakifanya kwa urahisi.
Mauzo siyo rahisi, yachukulie ni kazi inayohitaji kazi..

Hatua ya kuchukua leo; weka juhudi kubwa sana kwenye mauzo.
Jifunze njia mbalimbali za ukamilishaji wa mauzo.
Fanya mazoezi mengi ili mteja anapokuja unakuwa unaweza kukabiliana naye.

Kauli mbiu yetu; ABC: ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment