Kwenye maisha siri ya kupata ni kutoa. Mafanikio yoyote duniani yanakuja kwa njia ya kutoa.
Huwezi kupata kile unachotaka kama hujatoa. Ukitaka kitu ambacho huna unatoa hela na hela inakusaidia kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Kama unataka ng’ombe wako atoe maziwa mengi, basi mshibishe vizuri na utapata maziwa mengi.
Kwa chochote kile unachotaka kupokea, lazima utoea kwanza. Hii ni sheria ya kusababisha na matokeo (cause and effect).
Ili uweze kuimarisha mahusiano yako na mteja wako, hakikisha unafanya yafuatayo. Kwa kuwa mauzo ni mahusiano, unapohusiana na watu ndiyo unapata kile unachotaka.
Jinsi ya kuimarisha mahusiano yako na wateja wako;
Moja, mpe mteja dili nzuri. Unapompa mteja dili nzuri anakuwa tayari kuendelea kununua kwako. Hakuna mtu ambaye hataki dili nzuri la kumsaidia kupata fedha. Kwa mfano, kama mteja wako aliuziwa bidhaa za jumla kwa elfu kumi, na wewe ukamwonesha dili nzuri kwa kumpatia bidhaa ile ile kwa bei ya chini badala ya elfu ya elfu 10, ukampatia kwa elfu tano. Unafikiri siku nyingine akitaka kununua kitu atafikiria kwenda kwa mwingine? Hapana kwa sababu ulishampatia dili nzuri huko nyuma.
Msaidie mteja wako kupata koneksheni mbalimbali. Kama kuna koneksheni yoyote ile na unajua itamsaidia mteja wako mwambie. Usikae na koneksheni, toa na utapokea.
Msaidie mteja wako kufanya maamuzi. Kuna baadhi ya wateja wako wanashindwa kufanya maamuzi juu ya kitu fulani. Huenda hofu inawasumbua. Hivyo wewe kama mteja wasaidie wateja kufanya maamuzi pale unapoona wanakwama.
Ukijua mteja wako amesahau kufanya maamuzi msaidie kwa mfano, amepungukiwa na kitu mshawishi anunue zaidi.
Mpatie wateja wa rufaa. Kama una wateja ambao wanaweza kunufaika na biashara ya mteja wako ni vizuri ukampatia wateja. Unajua mteja wako anafanya kitu fulani ambacho wewe huna, mpendekezee kwa mtu mwingine na atakuja kukushukuru baadaye.
Shirikiana na wateja kwenye michezo na mambo ya kijamii. Kama unataka kujenga mahusiano bora na wateja wako na mahusiano kiujumla basi hakikisha mnashirikiana kwenye mambo ya kijamii na mteja wako.
Pia mshirikiane kwenye michezo. Jua timu ambayo mteja wako yupo au anapendelea kufuatilia michezo ya aina gani na kisha mshirikiane.
Kwa namna hii utafanikiwa sana kujenga mahusiano bora na wateja wako. Kila kitu ni mahusiano, unapohusiana na mteja wako vizuri lazima ataendelea kubaki na wewe na kutokwenda kwa mwingine.
Hatua ya kuchukua leo;
Mpe mteja dili nzuri.
Msaidie mteja wako kupata koneksheni mbalimbali.
Msaidie mteja wako kufanya maamuzi pale anapokuwa anakwama kwa sababu mbalimbali.
Mpatie mteja wako wateja wa rufaa ambao atawageuza na kuwa wateja kamili.
Hiki ni kionjo tu kutoka kwenye kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO. Ninakusihi uweke oda yako mapema, kwani watakaoweka oda yao mapema watapata punguzo. Kaa Kwenye orodha mapema ili upate zawadi pamoja na kitabu chako.
Ukijenga mahusiano na mteja wako, unatakiwa kuyaimarisha. Kwa sababu MAUZO NI MAHUSIANO, hauuzi mara moja, bali unamwitaji mteja uliyempata maisha yako yote ili aendelee kununua.
Mwisho, mauzo ni njia sahihi ya kuweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Mauzo ndiyo ushindi wa uhakika, ukipata umepata, hivyo usipange kukosa kusoma kitabu hiko, siyo tu kitakusaidia sana kwenye mauzo, bali pia kuboresha mahusiano yako, utakuja kunishukuru baadaye baada ya kukisoma kitabu hiko.
Naomba unisaidie kitu kidogo, naomba unisaidie kuisambaza makala hii kwa mtu wako mmoja tu unayempenda ambaye unataka naye aje kunufaika kama utakavyonufaika wewe na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO.
Hatua ya kuchukua leo; weka oda yako sasa hivi kwenda namba 0717101505 ili ujihakikishie nafasi ya kupata kitabu kwani watu wengi wameweka oda.
Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz
1 Comment
HOSEA JORDAN
Thank you so much