Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Jinsi Ya Kumshawishi Mteja Kununua Zaidi Huduma Yako

Je, umewahi kusikia usemi wa mteja ni mfalme? Naam! Kama tayari hongera, kama bado karibu. Hapa utapata dondoo zaidi ya namna gani unapaswa kumchukulia mteja kama mfalme. Lengo ni kumshawishi zaidi kununua huduma yako.

Kama tunavyojua mfalme ni mtawala wa nchi fulani ambaye ananyenyekewa. Sauti yake inasikika na anapewa kila kitu anachopenda. Pia, anaamua vile apendavyo.

Kwenye mauzo pamoja na mambo mengi unayofanya dhana hii ya mteja ni mfalme tukiibeba itatuongezea ufanisi na kukuza mauzo yetu. Badala ya kuwapa kile unachotaka unawapa kile wanachotafuta.

Dhana ya mteja ni mfalme inaonyesha thamani kubwa aliyonayo mteja katika biashara yako. Hii ni kwa sababu kupitia manunuzi anayofanya, namna anavyoitangaza biashara yako anaifanya isimame imara na kukua.

Wela akilini kwamba kwenye biashara bila mteja hakuna mauzo na kama hakuna mauzo basi hakuna biashara au huduma. Ili kufanikisha hili unahitaji wateja kwa hali na mali

Hivyo, pambana sana kutoa huduma nzuri kwa wateja kwa sababu wananunua huduma, sio bidhaa. Bidhaa hupatikana kila mahali, lakini huduma ndio huleta utofauti. Hapa chini kuna mambo ya kuzingatia ili kuwashawishi wateja wako na kuwauzia zaidi;

Moja; Toa Huduma Bora Zaidi.

Kama nilivyoandika hapo awali wateja wanapenda huduma nzuri. Na ndiyo inayokutofautisha wewe na wauzaji wengine. Ni kupitia huduma bora, wanaiona thamani kubwa kwako.

Kwa kuwa wateja kwako ni muhimu sana na wafalme wako basi wape kile wanachopenda. Weka nguvu matakwa yao na sio yako, utawashawishi wengi zaidi kuchukua hatua.

Mbili; Ijue Nguvu Ya Wateja.
Waridhishe wapate kile wanachopenda. Wateja Wana nguvu sana katika zama hizi. Ukiwajali wataipenda biashara yako na kuitangaza.

Usipowajali hawataipenda biashara yako, badala yake wataikimbia na kuichafua kupitia kwenye mtandao ya kijamii. Kitu kilichokuwa tofauti zamani. Huko walikuwa wanafanya migomo na kutokuja kabisa katika biashara yako.

Tatu; Usiwalazimishe Wateja Kununua

Kumbuka, mfalme ni mtawala anayesikilizwa na kunyenyekewa. Sio mtu anayependa kulazimishwa. Anapenda kuona sauti yake inasikika Kila mahali.

Ipo hivyo kwa wateja wako. Unapaswa kufuata matakwa yao. Usiwaambie moja kwa moja Acha hiki, chukua hiki. Nunua sasa na mengine mengi. Wanaheshimu washauri wao.

Tumia maneno ya ushawishi kuteka umakini wao. Lakini sio kuonekana moja kwa moja unawalazimisha kununua bali wasaidie kufanya maamuzi.

Nne; Tatua Maumivu Zao.
Fanya inteligensia kujua tatizo linalowakabili ili uguse hisia zao. Hii ni kwa sababu hisia za mteja zimejificha kwenye maumivu yake. Fanya hima kuyagundua ili Kuwapa kilicho bora.

Namna nzuri kujua maumivu yake, kuwa nao karibu. Waulize maswali rahisi. Kupitia maswali utayajua mengi kuhusu wao na utapata nafasi ya kuwashawishi.

Tano; Wape Uhuru wa Kuchagua.
Sisi binadamu tunapenda kuamua au kuchagua kitu tunachopenda. Mtu anapofanya machaguo mwenyewe anapata furaha, hata kama kutatokea changamoto sio rahisi kulalamika.

Jukumu lako ni kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi katika kufanya machaguo. Katika hili usiwape machaguo mengi. Wastani wape machaguo chini ya manne au matatu na sio zaidi.

Muhimu; Kitu kinachowakitanisha na wateja ni bidhaa uliyonayo. Jitahidi kuijua vema ili umpe thamani kubwa mfalme wako. Ndiye anafanya biashara yako kusimama.

Mara zote mteja muone kama mfalme. Yajue mahitaji yake, pokea mrejesho wake, mpe huduma nzuri, mfanye aikumbuke biashara yako, fanya maboresho panapohitajika. Mwisho, usikubali kupitwa na pesa yake.

Je, unawahudumia vizuri wateja wako? Bonga nasi hapa hapa.

Kwa mafundisho zaidi pata kitabu Cha MAUZO NI HUDUMA Ndani yake kimeelezea mengi kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja wateja, kuomba rufaa na kuwabakiza Katika biashara yako milele.

Makala imeandaliwa na Lackius Robert, Mwandishi wa vitabu na Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo. Karibu tuwasiliane kupitia 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Hakika, mauzo ni huduma.
Karibu tujifunze na kuuza zaidi
Karibuni.

Leave a comment