Habari njema ni kwamba, kila mtu anapenda kupata faida. Kila mtu anapenda kuongeza mauzo kama anafanya biashara.
Kila mtu anapenda kupata matokeo mazuri zaidi. Na mauzo ndiyo moyo wa biashara. Kwa sababu, kupitia mauzo kila kitu kinapatikana.
Kama mauzo yakiongezeka, utapata mapato makubwa, utajilipa vizuri, utawalipa wasaidizi wako vizuri.
Utafanya maendeleo kwenye biashara yako.
Wote tunajua kwamba, fedha ni mfalme. Fedha ikiwepo kwenye biashara kila kitu kinaenda vizuri.
Sina uhakika kama itakufaa lakini fedha ndiyo jawabu la mambo yote. Biashara ikiwa na fedha, itapendeza.
Pata picha kama unataka kuongeza mauzo kwenye biashara yako mtu wa kwanza wa kumfikiria wa kukusaidia kufanya hivyo atakua nani?
Mtu wa kwanza wa kukusaidia kuongeza mauzo yako ni mteja wako ambaye ananunua kwa sasa kwenye biashara yako.
Waswahili wanasema, fimbo ya mbali haiui nyoka. Mteja anayenunua kwako, ndiyo mgodi wa dhahabu ambaye atakupa mauzo makubwa.
Nini kifanyike ili wateja wako wakusaidie kuongeza mauzo?
Wateja wetu ni kama wapenzi wetu. Wapenzi wetu hawawezi kutupa mapenzi mazuri na kufurahia kama hatuna mahusiano mazuri na wapenzi wetu.
Kumbe basi, ili wateja wako waweze kununua zaidi kwako, unapaswa kwanza kuwa na mahusiano mazuri na wateja wako.
Kama huna mahusiano mazuri na wateja wako hawawezi kununua kwako zaidi. Hawawezi kurudi tena kununua.
Hawawezi kukuletea wateja wa rufaa.
Hawawezi kukusemea mazuri kwa watu wake wa karibu.
Umeona mahusiano mazuri na wateja wako yalivyokuwa na nguvu?
Ili ng’ombe wako atoe maziwa mengi, lazima umlishe vizuri.
Na majani ambayo unapaswa kumlisha mteja wako ni kuwa na mahusiano mazuri tu.
Mahusiano mazuri na mteja wako, yatakuongezea mauzo. Watu wananunua kwa watu wanaowapenda, ili watu wakupende lazima uwe na mahusiano mazuri na watu hao.
Je, utawezaje kujenga na kuimarisha mahusiano yako na kumfanya mteja wako kuwa wako daima na kununua zaidi?
Habari njema ni kwamba, kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO, kipo tayari, kuanzia wiki ijayo kitaanza kuuzwa.
Watu wengi wameshaweka oda, na sidhani kama utapata kitabu kama bado hujaweka oda yako mpaka sasa kwa sababu watu wengi tayari wameweka oda na tumezalisha nakala chache.
Piga simu au tuma ujumbe sasa hivi kwenda namba 0717101505/0767101504 kuweka oda yako sasa ili kinapozinduliwa wiki ijayo uwe wa kwanza kupata nakala yako bila KUKOSA.
Kitu kimoja zaidi, MAUZO NI MAHUSIANO na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO kinakwenda kukusaidia kukupa mbinu za kumfanya mteja wako kuwa wako daima.
Nani asiyependa kuwa na mteja wake daima?
Na kitabu kitauzwa kwa shilingi elfu 20.
Habari njema ni kwamba siyo tu kitakusaidia kujenga mahusiano na wateja wako lakini pia hata mpenzi wako, watoto au wale wote ambao unahusiana nao. Ukitumia mbinu hizi, utakuja kunishukuru baadaye.
Mwisho, mauzo ni njia sahihi ya kuweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Mauzo ndiyo ushindi wa uhakika, ukipata umepata, hivyo usipange kukosa kusoma kitabu hiko, siyo tu kitakusaidia sana kwenye mauzo, bali pia kuboresha mahusiano yako, utakuja kunishukuru baadaye baada ya kukisoma kitabu hiko.
Naomba unisaidie kitu kidogo, naomba unisaidie kuisambaza makala hii kwa mtu wako mmoja tu unayempenda ambaye unataka naye aje kunufaika kama utakavyonufaika wewe na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO.
Hatua ya kuchukua leo; weka oda yako sasa hivi kwenda namba 0717101505 ili ujihakikishie nafasi ya kupata kitabu kwani watu wengi wameweka oda.
Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz