Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mbinu Tatu Za Ukamilishaji Wa Mauzo 5-7

Habari njema muuzaji bora kuwahi kutokea,

Mafanikio ya mtu kifedha na kwenye maisha kwa ujumla yanategemea sana uwezo wake wa kukamilisha au kupata kuungwa mkono na wengine kwenye kile anachofanya.

Kama ni wazo basi kuungwa mkono na watu sahihi na kama ni bidhaa basi kununuliwa na wateja wanaolengwa.

Kwa maana hiyo, ukamilishaji unaweza kuitwa mabadilishano ya ushindi, kila mtu anapata ushindi fulani. Muuzaji anapata fedha, mnunuaji anapata thamani kupitia bidhaa au huduma aliyonunua.

Leo ikiwa ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA , tunakwenda kujifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo.

Leo tunakwenda kujifunza mbinu namba 5,6 na 7.

5. Ukamilishaji wa jina/usajili.

Hii ni aina ya ukamilishaji ambapo muuzaji anadhania kwamba mteja ameshakubali kwa kumuuliza kile anachonunua jina tunaandika nani.

Mteja ukimuuliza jina la bidhaa tuandike nani, akishakutajia jina maana yake tayari ameshakubaliana na kile unachomuuzia hivyo kinachofuata baada ya hapo ni wewe kukamilisha mauzo tu.

Kwa mfano unamwambia mteja,

Ni jina la nani litaandikishwa kwenye bidhaa yako?
Ni jina la nani litaandikishwa kwenye mkataba wako wa kiwanja?
Jina lako, la mke wako au yote mawili?
“Ni jina la nani litaandikishwa kwenye ____ yako? Jina lako, la mke wako au yote mawili?”

Ufafanuzi; huu ni ukamilishaji wa kudhania wenye nguvu, unapaswa kumwangalia mteja machoni kwa kujiamini wakati unamuuliza swali hilo.

6. Ukamilishaji wa makubaliano.
Huu ni sawa na ukamilishaji wa jina/usajili, ila huu umejikita kwenye mchakato wa makubaliano.

Ukamilishaji huu namba sita, unasaidia kujua nguvu ya mtu kwenye kufanya maamuzi

Kwa mfano unamuuliza mteja,
“Ni jina la nani litatumika kwenye karatasi za makubaliano, jina lako, la kampuni au yote?”

Ukamilishaji huu unatumika sana kwenye utoaji wa huduma kama vile mawakili.
Hata wauzaji wa viwanja, magari, nyumba na nk.

Unatumia ukamilishaji huu kwa kudhania kwamba mteja tayari ameshakubaliana na wewe hivyo wewe unamuuliza hivyo kuthibitisha jina na kisha unakamalisha mauzo.
Mtu akishakuwa tayari kukuambia jina litakalotumika kwenye huduma au bidhaa unayouza maana yake tayari ameshakubaliana na kile unachouza.

7. Ukamilishaji wa kuongea na mwenza – 1.

(Pale mtu anaposema inabidi aongee na mwenza wake kwanza kabla ya kuamua)

“Vipi kama mwenza wako atakataa?” Akijibu, hawezi kukataa, mwambie; “Vizuri, weka sahihi hapa. hapa mteja anaweka sahihi kama biashara au huduma unayotoa inahusiana na kuweka sahihi

” Akijibu atakataa, muulize; “Je atakataa bidhaa au bei?” Kama bidhaa; “Nini mapendekezo yako?”
Kama fedha; “Nini atakataa kwenye fedha, bei au mpango wa malipo?”

Kitu kimoja zaidi, wengi huwa wanatumia kuongea na mwenza kama kisingizio cha kukwepa kufanya maamuzi. Unapouliza maswali ya kujua zaidi, huwa wanafikia kufanya maamuzi. Watu wakikikubali kitu huwa wanakinunua na kwenda kukitetea kwa wenza wao.

Hatua ya kuchukua leo; chagua mbinu moja kati ya hizi za ukamilishaji wa mauzo, nenda kazifanyie kazi na kisha uje ushuhudie matokeo mazuri uliyopata.

Usiseme haifanyi kazi kabla hujaifanyia kazi.
Timiza wajibu wako, na kisha acha wengine nao watimize wajibu wao, 
Kaa kwenye mchakato, hakikisha mara zote unawakamilisha wateja.
Na ukamilishaji ndiyo unaoleta fedha mfukoni kwako.
Mauzo ndiyo moyo wa biashara, hakikisha moyo wa biashara yako unadunda muda wote.
Ukisimama biashara inakufa.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment