Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mteja Kamili Na Namna Nzuri Kumbakiza Katika Biashara Yako

Mteja Kamili
Huyu ni mtu ambaye amenunua kitu kutoka kwa muuzaji kwa mara ya kwanza. Yaani, amefanya mabadilishano ya pesa na muuzaji kupewa bidhaa au huduma.

Kama ni bidhaa anainunua na kuanza kuitumia. Kama ni huduma anasaini mkataba na kuanza kuhudumiwa. Mteja ambaye hajatoa pesa yake, huyo siyo kamili. Maana huwezi kutumia pesa yake. Lakini mteja kamili, unaweza kutumia pesa yake. Hata kama akilipia pesa ya kianzio, huyo ni mteja kamili.

Sifa za Mteja Kamili;
Moja; Ametoa pesa yake mfukoni kufanya malipo.
Mbili; Makubaliano ya pande mbili.

Mauzo ni mchezo kama zilivyo michezo mingine. Uwanja wako ni eneo lako la huduma au biasharabyako. Mpinzani unayeshindana naye ni mteja wako.

Mpira wa miguu mchezaji anapiga chenga uwanjani. Kwenye mauzo, muuzaji anamshawishi kwa maneno na ushawishi kumuuzia bidhaa.

Kwenye mpira wa miguu magoli ndiyo ushindi. Kwenye mauzo, pesa anayotoa mteja kuchukua bidhaa yako ndiyo ushindi mkuu.

Kama zilivyo timu kabla ya mechi majigambo huwa ni mengi lakini moyoni kunakuwa na hamasa ya kupambana zaidi kuhakikisha wanapata ushindi wa pointi tatu. Huwezi kupata pointi tatu kama hujashinda mchezo. Hata kwenye mauzo ipo hivyo, bila mteja kutoa pesa yake huwezi kujinadi kwamba umemshinda.

Kwenye mauzo kuna kuuza na kuuziwa. Mteja anakuuzia sababu pale anapokukatalia kununua. Na wewe unamuuzia bidhaa pale anapokubali kulipia pesa yake. Hata kwenye mchezo wa mpira ipo hivyo, kuna kushinda na kushindwa.

Kinachoongezeka ni sare, kitu ambacho hakipo kwenye mauzo. Yaani kusema, ilibaki kidogo nimuuzie sema basi usiku umeingia au bidhaa imeisha. Kwenye mauzo kuna matokeo ya aina mbili, kuuza na kuuziwa, basi.

Kazi yako kama muuzaji ni kuhakikisha mteja anayefika kwenye biashara yao au kukutana naye analipia pesa yake. Usikubali kuruhusu akupe mabega. Pambana unavyoweza kuhakikisha unadhibiti mapingamizi yake ili ukamilishe mauzo. Kupitia kukamilisha mauzo ndipo unapata mahitaji yako.
Kitu kinachokuweka kwenye biashara ni kuuza. Hakuna kitu kingine.

Kumbuka mengine yote kufanya usakaji, ushawishi, urafiki, huduma nzuri yote ni chenga, fainali ni mteja kutoa pesa yake. Kupitia pesa unayopata kutoka kwa mteja ndipo tunapima ufanisi wako. Maana mauzo ndiyo moyo wa biashara. Ikumbuke hii mara zote ili uzidi kutengeza wateja zaidi.

Baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati wa ukamilishaji;
Moja; Kumkaribisha mteja, kumsifia, kumsikiliza na kujua hitaji lake.

Mbili; Kuuliza maswali
Tatu; Kuongea sauti inayosikika(shauku) na kutabasamu
Nne; Kumpatia mfano, ushuhuda na kumuuzia.
Tano; Kufanya mauzo ya ziada, kuomba mawasiliano na rufaa

Baada ya mteja kununua mtumie ujumbe wa shukurani ndani ya saa 24 au saa 48. Muandikie hivi;

“Pongezi kubwa Mr/Miss J..kwa manunuzi uliyofanya kwetu, tumefurahi kuungana na wewe. Tafadhali tuma mrejesho wako hapa kuhusu huduma zetu”.

”Habari (J) kampuni ya (W) unapenda kukushukuru kwa manunuzi uliyofanya leo. Tafadhali fuatilia tarehe fulani kuona ujio wa mzigo mpya”.

“Hongera Mr/Miss J.. kwa kuuona mwezi au mwaka mpya. Kampuni ya (W) tunafurahi kutuchagua na kufanya biashara na sisi. Timu yetu imedhamiria kukusaidia kufikia (Malengo) na tupo tayari kwenda pamoja na wewe”.

Mteja aliyefanya malipo kidogo;

“Asante Mr/Miss kwa kufanya malipo ya awali. Malipo ya mwisho yatafanyika tarehe fulani. Tunakupenda na kukujali”

Baada ya mteja kuona ujumbe na kukujibu (mrejesho) mjibu hivi;

“Asante sana Mr/Miss J kwa kushirikisha mrejesho wako. Tunaahidi kuufanyia kazi”.

“Shukurani sana Mr/Miss J kwa mrejesho wako wa thamani. Tunaahidi kutekeleza yote uliyo shauri”.

Umuhimu wa kumshukuru mteja;

Moja; Kwa ajili ya kupata rufaa
Mbili; Kumbakiza katika biashara yako
Tatu; Kuonyesha upekee kwenye huduma au biashara
Nne; Kumfanya ajisikie vizuri.
Tano; Kumthamini mteja.

Zingatia kuthibiti mazungumzo wakati wa ukamilishaji wa mauzo.

Fanyia kazi yote uliyojifunza katika somo la leo.

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi.
0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi

Leave a comment